Mpanda FM
Mpanda FM
6 August 2025, 2:21 pm

Picha ya bodaboda zilizoegeshwa kwenye moja ya kituo. Picha na Roda Elias
“Wenyeviti wa vijiwe watilie mkazo jambo hili”
Na Roda Elias
Madereva pikipiki maarufu kama bodaboda wa kata ya Mpanda Hotel manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuwa na umoja na mshikamano.
Akizungumza na Mpanda Radio FM mwenyekiti msaidizi wa kanda ya Mpanda Hotel Steven Nsilya amesema kuwa idadi ya bodaboda wanaojitoa katika matatizo ya wenzao ni ndogo kwani hakuna ushirikiano.
Aidha Nsilya amewataka wenyeviti wa kila kijiwe kuweka mkazo kwa madereva hao na wakikaidi wenyeviti wa vijiwe watoe taarifa ngazi za juu.
Kwa upande wao baadhi ya madereva wa bodaboda wametoa maoni yao juu ya suala la kutokutoa michango huku wakidai kuwa kukosekana kwa upendo ndio chanzo.
kwa upande wake mwenyekiti wa madereva bodaboda mkoa wa Katavi Isack Joseph amekiri kutoa wito kwa madereva kusaidizana katika shida na raha ili kuwa na mshikamano.