Mpanda FM

Wajumbe wawang’oa vigogo kura za maoni Katavi

6 August 2025, 12:43 pm

Katibu mwenezi wa CCM Theonas Kinyonto akisoma matokeo ya kura za maoni ya ubunge. Picha na Anna Mhina

“Kura za maoni ni mchakato wa kuwapata wagombea watakaoipeperusha bendera ya CCM”

Na Anna Mhina

Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Katavi kimetoa rai kwa wanachama wa chama hicho kuwa watulivu, kuimarisha umoja na mshikamano ili kuruhusu michakato ya kikatiba ndani ya chama kuendelea.

Hayo yamesemwa na katibu mwenezi wa CCM mkoa Theonas Kinyonto alipokuwa akisoma matokeo ya kura za maoni ya ubunge za majimbo yote matano ambapo Beda Katani ameongoza kura za maoni katika jimbo la Mpanda mjini huku aliyekuwa mbunge wa jimbo la Kavuu na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Geofrey Pinda akianguka katika mchakato huo.

Sauti ya mwenezi wa CCM mkoa

Katika hatua nyingine Kinyonto amewataka wanachama kuwa watulivu kwani kura za maoni ni moja ya mchakato unaofanyika ndani ya chama ili kuweza kuwapata wagombea watakaoipeperusha bendera ya chama hicho.

Sauti ya mwenezi wa CCM mkoa

Zoezi hilo la kutangazwa kwa matokeo ya kura za maoni ya ubunge kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Katavi limefanyika Augost 5,2025 katika ofisi za CCM mkoa.