Mpanda FM

Walioteuliwa udiwani wawekwa wazi, Ilembo na Uwanja wa ndege out

30 July 2025, 7:25 pm

Katibu wa siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Theonas Kinyoto. Picha na Samwel Mbugi

“Kata ya Mpanda hotel namba moja ni Oscar John Mbule”

Na Samwel Mbugi

Katibu wa siasa na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Theonas Kinyoto ametangaza majina ya walioteuliwa kwenda kupigiwa kura za maoni kupitia kata zote za mkoa wa Katavi.

Hayo yamejiri katika ofisi za CCM mkoa akizungumza na wandishi wa habari, ambapo amewataja watia nia ya ugombea udiwani katika kata 58 kwa mujibu wa katiba ya chama hicho, Kwa baadhi ya kata mbazo amezitaja  zilizopo manispaa ya Mpanda ni pamoja na Mpanda Hotel.

Sauti ya katibu mwenezi

Kinyoto pia amewataja watia nia ya kugombea udiwani wa kata mbalimbali kutoka wilaya ya Mlele na Tanganyika kupitia chama cha mapinduzi ikiwemo kata ya Mamba na Kabungu.

Sauti ya katibu mwenezi

Ikumbukwe kuwa hayo ni baadhi ya majina yaliyoteuliwa na kamati ya siasa ya CCM kutoka kata zote 58 za mkoa wa Katavi kwa ajili ya kwenda kushiriki kura za maoni kwa nafasi ya udiwani.