Mpanda FM

Masanja ajitosa ubunge jimbo la Mpanda mjini kupitia CHAUMA

24 July 2025, 11:04 am

Masanja akiwa amekabidhiwa fomu ya kugombea ubunge. Picha na Benny Gadau

“Jimbo la Mpanda mjini ni jimbo la wanamageuzi”

Na Benny Gadau

Kamishna wa kanda maalum ya magharibi wa Chama Cha Ukombozi wa Umma CHAUMA Masanja Musa Katambi amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mpanda Mjini kupitia chama hicho.

Akizungumza wakati akikabidhiwa fomu hiyo Masanja amesema kuwa dhamira yake ni kuhakikisha anawaletea maendeleo wananchi wa Jimbo la Mpanda Mjini huku akiwataka wananchi na wanachama wa chama hicho kuendelea kumuunga mkono.

Sauti ya Masanja

Kwa upande wao baadhi ya wanachama wa chama hicho cha Ukombozi wa Umma CHAUMA wamesema kuwa wanaimani na mgombea wao katika nafasi hiyo ya Ubunge huku wakisema kuwa watahakikisha wanamuunga mkono kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Sauti za wananchi

Katika hatua nyingine Masanja amezindua ofisi ya chama hicho cha Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA) zilizopo katika kata ya kashaulili manispaa ya Mpanda mkoani Katavi.