Mpanda FM
Mpanda FM
24 July 2025, 10:47 am

Picha ya pamoja ya viongozi wa mradi, katikati ni mkuu wa wilaya ya Tanganyika. Picha na Anna Millanzi
“Kila fedha inayotengwa kwa miradi imelenga kuimarisha ustawi wa jamii”
Na Anna Millanzi
Katika kuhakikisha usimamizi wa rasilimali za umma na uwajibikaji unaongezeka kwa wananchi na viongozi wilayani Tanganyika mkuu wa wilaya hiyo amezindua mradi wa raia makini.
Mradi huo wa Raia makini unatekelezwa na taasisi mbili zisizokuwa za kiserikali ikiwemo Tosovic na Tupafo huku mradi huo ukiwa umekuja kwa dhumuni kuhimarisha uwajibikaji na uwazi kwa wananchi.
Wakizungumza wakati wakiwasilisha risala za taasisi hizo mbili Bwanali Kondowe mkurugenzi kutoka taasisi ya TUPAFO na George Kasabwe katibu mtendaji TOSOVC ambaye alimwakilisha mkurugenzi wa Taasisi hiyo wameeleza maeneo ambayo mradi huo utatekelezwa.
Mkuu wa wilaya ya Tanganyika akiwa anazindua mradi huo amewasisitiza watumishi wa serikali kusimamia vyema rasilimali za umma ili mthibiti na mkaguzi mkuu wa serikali CAG atakapopita wakati ujao kusiwe na dosari yoyote itakayo jitokeza wilayani humo.
Wadau waliohudhuria katika uzinduzi huo ikiwemo watendaji wa kata ,vijiji pamoja na wenyeviti wa vijiji ambao mradi huo wa raia makini unaokwenda kutekelezwa wameeleza namna ambavyo wamepokea maagizo na kuahidi kuyafanyia kazi.
Mradi wa Raia makini unaotekelezwa na Taasisi hizo mbili wilayani Tanganyika ni mradi unaotokana na taasisi ya wajibu wakishirikiana na Policy Forum huku mradi huo ukifadhiliwa na Umoja wa Ulaya