Mpanda FM

Mafua tishio Katavi

21 July 2025, 3:21 pm

Dr. Masalagwe Gambishi.Picha na Anna Mhina

“Kwenye hali ya hewa ya baridi kuna kirusi kinachosababisha mafua”

Na Anna Mhina

Wananchi mkoani Katavi wameshauriwa kunywa maji mengi, kuvaa nguo nzito na kuvaa barakoa katika kipindi hiki cha baridi ili kuepuka kuugua mafua ya mara kwa mara na kifua kisichokoma.

Akizungumza na Mpanda radio FM Masalagwe Gambishi ambaye ni daktari kitengo cha dharura katika hospital ya rufaa mkoa wa Katavi amesema changamoto ya watu kuugua magonjwa ya mafua na kifua katika kipindi hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa inasababishwa na uwepo wa bakteria aina ya influenza.

Sauti ya daktari

Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda wamewaomba wataalamu kuwapa elimu ya namna ya kuepukana na mafua na hatua za kufuata ili kuendelea kujikinga.

Sauti ya wananchi

Mafua yanaweza kuonekana ya kawaida lakini husababisha matatizo makubwa ya mapafu na kushindwa kupumua hivyo ni vema kufika kituo cha afya kwa ajili ya matibabu.