Mpanda FM
Mpanda FM
19 July 2025, 5:36 pm

Stewart Kiyombo Kaimu mkurungezi TAKUKURU Katavi. Picha na Blessing Kikoti
“Wananchi waunge mkono vita dhidi ya rushwa ya kisiasa”
Na Blessing Kikoti
Uwepo wa rushwa katika jamii mkoani Katavi umetajwa kusababisha wananchi kuchagua viongozi wasiostahili na wasiokuwa na weledi katika utekelezaji wa majukumu yao katika jamii.
Hayo yamebainishwa na kaimu katibu Tawala mkoa wa Katavi Florence Chrisant katika mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoa wa Katavi Takukuru ambayo yalikuwa yamelenga viongozi wadini, wakimila na wazee maarufu.
Stewart Kiyombo Kaimu mkurungezi Kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Katavi amesema kuwa mapambano ya kuzuia rushwa si kazi ya TAKUKURU pekee bali ni ya jamii nzima hivyo ameiomba jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa juu ya vitendo hivyo.
Kwa upande wao baadhi ya washiriki katika mafunzo hayo wameishukuru TAKLUKURU mkoa wa Katavi kwa kuandaa mafunzo ambayo yamewapatia elimu itakayoisaidia jamii katika mapambano dhidi ya rushwa.
Taasisi ya kuzuia na kupamba na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Katavi imeendesha mafunzo hayo wakati Tanzania ikiendelea kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October mwaka huu.