Mpanda FM

Wananchi Katavi walalamika kutopata mkopo

17 July 2025, 2:12 pm

Baadhi ya wananchi walioahidiwa mkopo. Picha na Samwel Mbugi

“Tangu tulipokabidhiwa hundi mpaka sasa hela hazijaingizwa bank”

Na Samwel Mbugi

Baadhi ya wananchi ambao ni wanufaika wa mkopo wa asilimia kumi wametoa malalamiko yao kwa serikali kutopata mkopo huo ambao waliahidiwa baada ya kupokea hundi ya mfano.

Wakizungumza na Mpanda Radio FM wamesema kuwa waliahidiwa kupata mkopo huo siku ya kupokea hundi ila mpaka sasa hawajapata.

Sauti ya wanufaika

Kwa upande wake mratibu wa mikopo hiyo Rozina Ngonyani amesema kuwa hawezi kutoa majibu ya nini kimekwamisha kwa sababu mwandishi wa habari sio mwanakikundi .

Sauti ya mratibu

Hata hivyo mkurugezi wa manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli amesema kuwa mchakato huo unaendelea kufikia wiki  ijayo kila kitu kitakuwa sawa.

Sauti ya mkurugenzi

Ikumbukwe kuwa vikundi vilivyokidhi vigezo kwa ajili ya kupata mkopo huo ni 86 kati ya 126 vitanufaika na mkopo huo ambao ni milioni 839,725,000/=.