Mpanda FM
Mpanda FM
14 July 2025, 2:29 pm

Mkuu wa Dawati la Jinsia Katavi Judith Mbukwa. Picha na Anna Mhina
“Mazingira yenyewe ya ndani yanasababisha kukimbia familia”
Na Leah Kamala
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamesema kuwa hali ngumu ya kimaisha na changamoto ya kimahusiano imepelekea wanaume wengi kutelekeza familia zao.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa mazingira duni ya maisha yanaweza kupelekea familia nyingi kusambaratika.
Mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa Katavi Judith Mbukwa amesema kuwa wanaume wengi wanatelekeza familia kutokana na kipato duni cha familia amewashauri wazazi kushirikiana kwa pamoja katika kuhudumia familia
Ili kupunguza tatizo hili ni muhimu kuwepo na elimu, ushauri nasaha, malezi bora na msaada wa kijamii ili wazazi wajifunze kuwajibika na kutimiza majukumu yao.