Mpanda FM
Mpanda FM
8 July 2025, 7:56 pm

Mwalimu Benjamin Chahe kutoka chuo Mkwawa V.T.C Iringa. Picha na Anna Mhina
“Leo nimefurahi mchele kumbe ni sabuni!”
Na Anna Mhina
Wajasiriamali ambao wanapatiwa mafunzo ya ufugaji bora wa kuku, utengenezaji wa sabuni na batiki wameonesha kufurahia mafunzo ya utengenezaji wa sabuni ya mchele.
Wakizungumza na Mpanda radio FM baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Marietha Ezekiel na Abeli Katumbo wameeleza namna walivyofurahia somo la utengenezaji wa sabuni ya mchele.
Benjamin Chahe ni mwalimu wa ujasiriamali na uchumi ameeleza faida za sabuni ya mchele ikiwa ni pamoja na kutibu magonjwa ya ngozi.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Mpanda radio FM kwa kushirikiana na chuo Cha Mkwawa VTC kilichopo Iringa mjini yanatarajiwa kutamatika Julai 9,2025.