Mpanda FM
Mpanda FM
5 July 2025, 4:35 pm

Picha ya wananchi walionufaika wa mkopo wa asilimia 10. Picha na Samwel Mbugi
“Tunamshukuru Rais Samia kwa kuweza kutuona sisi vijana”
Na Samwel Mbugi
Baadhi ya wananchi manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi ambao ni wanufaika wa mkopo wa asilimia 10 wameishukuru serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali na kuwapa mkopo.
Wameyasema hayo wakati wa zoezi la kukabidhiwa Hundi wanufaika ambao ni wanawake, vijana na watu wenye ulemavu katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda
Awali akisoma taarifa mbele ya mgeni Rasmi Irene Samson Kileo ambae ni mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii manispaa ya Mpanda amsema vikundi vilivyokidhi vigezo ni 86 kati ya 126 vitanufaika na mkopo huo ambao ni milioni 839,725,000/=.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph ambae alikuwa mgeni rasmi amesema kuwa vikundi ambavyo bado havijapata mkopo visivunjike moyo atahakikisha navyo vinapata kwa awamu nyingine.
Jamila ameongeza kuwa mkopo huo ukatumike kama walengwa walivyoomba na kurejesha kwa wakati ili wananchi wengine waweze kunufaika