Mpanda FM

Vijana wa De Jong watua Katavi

5 July 2025, 4:25 pm

Vijana wa De Jong katikati ni afisa uhifadhi mwandamizi Shigela Jilala. Picha na Anna Mhina

“Tumetoka Zanzibar tumekuja Katavi kwa lengo la kuazimisha Samia day”

Na Anna Mhina

Katika kuadhimisha Samia day mkoani Katavi vijana 69 wa De Jong kutoka Kizimkazi Zanzibar wamekuja mkoani hapa kwa ajili ya kuungana na Wanakatavi katika kuazimisha siku hiyo.

Wakizungumza na Mpanda radio FM walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Katavi mratibu wa Taasisi ya vijana wa De Jong Hassan Jabir ameeleza lengo la ujio wao mkoani hapa ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi ya maendeleo iliyofanywa na Rais Samia.

Sauti ya mratibu

Awali akitoa tarifa ya maendeleo yaliyofanywa na Rais Samia katika hifadhi ya Taifa ya Katavi afisa uhifadhi mwandamizi idara ya ujirani mwema Shigela Jilala amesema kuwa kwasasa wanapokea wageni wengi kutokana na maboresho ya miundombinu.

Sauti ya Shigela Jilala

Sasha na Hamisi Mkombe ni miongoni mwa vijana kutoka De Jong Kizimkazi Zanzibar wameeleza furaha yao ya kutambelea hifadhi ya Taifa ya Katavi.

Sauti ya vijana wa De Jong

Hata hivyo vijana hao wa De Jong wametembelea miradi ya maendeleo mbalimbali ikiwemo mradi wa maji wa miji 28, mradi wa umeme wa Grid ya Taifa, Ghala la kuhiofadhia chakula NFRA, hospital ya Rufaa pamoja na hifadhi ya Taifa Katavi.