Mpanda FM

Historia kuandikwa Samia Day Katavi

2 July 2025, 7:27 pm

Albert Msovela katibu tawala Katavi. Picha na Samwel Mbugi

“Lengo la tamasha la Samia day ni kumpongeza Rais Samia kwa kuleta fedha nyingi Katavi”

Na Samwel Mbugi

Wananchi mkoani Katavi wamehimizwa kushiriki tamasha la Samia Day ambalo limeandaliwa kwa ajili ya kutangaza mafanikio ya serikali yaliyopatikana kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa wa awamu ya sita.

Hayo yamesemwa na katibu tawala mkoa wa Katavi Albert Msovela wakati akizungumza na wandishi wa habari katika ukumbi uliopo ofisi za mkuu wa mkoa ambapo amesema tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya shule ya msingi Ingonga halmashauri ya wilaya ya Mlele.

Sauti ya katibu tawala

Msovela amesema lengo la kufanya tamasha hilo ni kumpongeza na kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake wa kuleta fedha nyingi kwa mkoa wa Katavi ambazo ni Trioni 1.3 zilizosaidia kutekelezwa kwa miradi mingi ya maendeleo.

Sauti ya katibu tawala

Tamasha hilo litafanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 04-05/07/2025 mgeni rasmi atakuwa mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko ambapo kauli mbiu ya tamasha hilo ni ‘’ASANTE RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN KWA FEDHA ZA MAENDELEO, KATAVI IMARA NA MAENDELEO IMARA’’