Mpanda FM

Mfumo dume unavyomwathiri mwanamke kuwania uongozi

1 July 2025, 12:38 pm

Picha ya wananchi wa kijiji cha Isinde. Picha na Anna Mhina

“Nakosa ujasiri wa kugombea kwa sababu tunatawaliwa na mfumo dume kwenye familia”

Na Roda Elias

Kuendelea kuwepo kwa mfumo dume miongoni mwa baadhi ya jamii kumetajwa kumuathiri mwanamke  katika kuwania nafasi za uongozi.

Wakizungumza na Mpanda radio FM wakazi wa kijiji cha Isinde kata ya Mtapenda halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wamesema mfumo dume unamfanya mwanamke kukosa hali ya kujiamini hata katika nafasi za uongozi.

Sauti ya wananchi

Kwa upande wake Abdala Shabani kiongozi wa mila katika kijiji hicho amesema kuwa zamani viongozi wa kimila wanawake walikuwepo kwa sababu maalumu na sio kuchaguliwa.

Sauti ya kiongozi wa kimila

Anna Shumbi ni afisa maendeleo ya jamii mkoa wa Katavi amewataka wanawake kujitambua na kujitokeza kuwania nafasi za uongozi huku akiwataka wanaume kuwashika mkono wanawake hao.

Sauti ya afisa maendeleo

Mfumo dume humaanisha utawala wa baba na hutumiwa kurejelea mfumo wa kijamii ambapo wanaume hudhibiti sehemu kubwa isiyo na uwiano ya nguvu za kijamii , kiuchumi, kisiasa, kidini na urithi.