Mpanda FM
Mpanda FM
1 July 2025, 11:57 am

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Isinde. Picha na Anna Mhina
“Mfumo dume unaanzia nyumbani hivyo tunakosa kujiamini”
Na Anna Mhina na Roda Elias
Kuendelea kuwepo kwa mfumo dume miongoni mwa baadhi ya jamii kumetajwa kumuathiri mwanamke katika kuwania nafasi za uongozi.
Wakizungumza na Mpanda FM wakazi wa kijiji cha Isinde kata ya Mtapenda halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi wamesema mfumo dume unamfanya mwananmke kukosa hali ya kujiamini hata katika nafasi za uongozi.