Mpanda FM

Wanawake Katavi wahamasishwa kuchukua fomu

1 July 2025, 11:24 am

Idd Kimanta Mwenyekiti wa CCM na kulia ni Joseph Mona mwenyekiti wa ACT. Picha na Ben Gadau

“Kumekuwa na mwitikio mdogo kwa upande wa wanawake”

Na Ben Gadau

Wanawake wametakiwa kujitokeza katika mchakato wa kuchukua fomu inayoendelea katika vyama mbalimbali mkoa Katavi.

Hayo yamejiri mara baada ya Mpanda radio FM kuzungumza na miongongoni mwa vyama vya siasa vinavyotarajia kushiriki katika uchaguzi mkuu October mwaka huu.

Akizungumza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Katavi Idd Kimanta amesema kumekuwa na mwamko wa watu kujitokeza  kuchukua fomu za udiwani na  ubunge huku kukiwa na mwitikio hafifu kwa kundi la wanawake na vijana.

Sauti ya mwenyekiti wa CCM

Kwa upande wake Joseph Mona mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mkoani Katavi amesema mchakato wa uchukuaji fomu katika chama hicho unaendelea akibainisha kuwa wamepata wagombea katika majimbo muhimu ikiwemo Mpanda Mjini, Tanganyika, Katavi na Kavuu na kata nyingi mkoani hapa.

Sauti ya mwenyekiti ACT Wazalendo

Katika hatua nyingine Almasi Ntinje mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma  CHAUMA Mkoani Katavi amesema watatangaza utaratibu kuhusu uchukuaji wa fomu mara baada ya kukamilika kwa mkutano mkuu unaotarajia kufanyika siku za hivi karibuni.

Sauti ya mwenyekiti ya CHAUMA