Mpanda FM
Mpanda FM
30 June 2025, 5:42 pm

Choo kinachowakera ya wananchi. Picha na Anna Mhina
“Hapa sisi tunapata shida na harufu ya kinyesi”
Na Anna Mhina
Baadhi ya wananchi wa kata ya Mpanda hotel manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelalamikia kero wanayoipata ya harufu mbaya ya choo kilicho karibu na kilabu cha pombe za kienyeji na jinsi inavyohatarisha afya zao.
Wakizungumza na Mpanda radio FM kwa nyakati tofauti wananchi hao wameongeza kuwa choo hicho cha Jirani yao ambaye ni muuzaji wa pombe za kienyeji kinatoa harufu kali na kipo katika mazingira hatarishi kwao na watoto wao.
Nae mmiliki wa choo hicho James Christopher amekiri kujua changamoto hiyo na kudai kuwa yupo katika mikakati ya ujenzi wa choo bora.
Ibrahimu Msanda ni mwenyekiti wa kata ya Mpanda hotel amekiri kupokea taarifa hizo za kutokuwepo kwa choo bora na kuwapa muda wapangaji wa eneo hilo hadi pale choo kitakapokamilika.
Kwa upande wake afisa afya wa m anispaa ya Mpanda Erick Kisaka amesema kuwa sheria zimewekwa wazi kwa wale ambao wataenda kinyume hatua za kisheria zitachukuliwa.
Mpaka sasa katika kata ya mpanda hotel, jumla ya kaya 40 zimepewa ilani ya onyo ili kuboresha vyoo vya kaya zao kwa lengo la kuepuka kuenea kwa magonjwa ya mlipuko.