Mpanda FM
Mpanda FM
28 June 2025, 5:32 pm

Picha ya pamoja ya viongozi wa serikali na wanufaika wa TASAF. Picha na Samwel Mbugi
“Tupende kuwashukuru viongozi na mama Samia”
Na Samwel Mbugi
Baadhi ya wanufaika wa mfuko wa kaya masikini TASAF wametoa shukurani kwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuwajali na kuwezesha kiuchumi.
Wameyasema hayo wakati wa kikao cha tathimini ya shughuli za TASAF kwa mwaka wa 2024/2025 kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Katavi ambapo wamesema mfuko huo umekuwa mkombozi kwa familia zao.
Katibu tawala mkoa wa Katavi Albert Msovela amesema kuwa wataendelea kuwatia moyo wanufaika wa TASAF kupitia msaada unaotolewa na mfuko huo kwa kuwahamasisha kujishughulisha na shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji na kilimo cha bustani.
Ikumbukwe kuwa mfuko wa TASAF ni kuongeza fursa za kujiongezea kipato na kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii kwa kaya za walengwa na kulinda maslahi ya watoto wao.