Mpanda FM

Waandishi wapigwa msasa Katavi

26 June 2025, 2:07 pm

Baadhi ya waandishi wa habari wakipatiwa mafunzo. Picha na Anna Mhina

“Mafunzo ya leo yatatusaidia katika kuandaa habari kwa umakini”

Na Anna Mhina

Zaidi ya waandishi wa habari 20 mkoani Katavi wamepatiwa mafunzo ya lishe bora pamoja na ukatili kwa lengo la kuwajengea uwezo katika kuhakikisha wanatoa elimu bora kwa jamii.

Akifungua mafunzo hayo yaliyoambatana na uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha lishe bora na kupambana na udumavu mkoani Katavi kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mpanda Leah Gawaza ambaye ni afisa tarafa Misunkumilo amewataka waandishi kushikamana katika kuhakikisha wanatokomeza vita hii.

Sauti ya mgeni rasmi

Alinanuswe Edward ni mwenyekiti wa mtandao wa waandishi wa habari unaojishughulisha na kupambana na ukatili na utunzaji wa mazingira ameeleza lengo la uwepo wa mtandao huo ni pamoja na kuelimisha jamii kuhusu vyanzo vya ulemavu na njia za kukabiliana na ulemavu.

Sauti ya mwenyekiti wa mtandao

Kwa upande wao baadhi ya waandishi wa habari ambao wamehudhuria mafunzo hayo akiwemo Restuta Nyondo na Alex Ngereza wameeleza namna walivyonufaika na mafunzo hayo.

Sauti ya waandishi

Mafunzo hayo na uzinduzi wa kampeni ya kuhamasisha lishe bora na kupambana na udumavu mkoani Katavi yamefanyika katika ukumbi wa Mpanda hotel na kuhudhuriwa na maafisa mbalimbali wa serikali.