Mpanda FM
Mpanda FM
20 June 2025, 3:49 pm

Watembea kwa miguu wakivuka barabara eneo la Machinjioni. Picha na Samwel Mbugi
“Makundi yote ya watumiaji barabara wachukue tahadhari”
Na Samwel Mbugi
Kutokana na uwepo wa ajali za mara kwa mara eneo la Machinjioni manispaa ya mpanda mkoani Katavi wananchi wameomba kuwekewa kivuko cha watembea kwa miguu eneo hilo.
Hayo yamesema wakati wakizungumza na Mpanda radio FM kuwa eneo hilo limekuwa likisababisha ajali nyingi ambazo zinatokana na mwendokasi kwa madereva na wananchi kutokuchukua tahadhari wakati wa kuvuka.
Kwa upande wake CPL Sophia Peleka kutoka jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani amesema kuwa chanzo cha ajali eneo hilo ni kutokuwa na elimu kwa wananchi pamoja na mteremko mkali uliopo eneo hilo.
Hata hivyo Peleka amesema kuwa ili kupunguza ajali zisizo na ulazima inapaswa wananchi pamoja na madereva kuchukua tahadhari.
Peleka amewataka madereva ambao hawana elimu ya udereva kwenda kusoma ili kujua sheria, miongozo na alama za barabarani.