Mpanda FM
Mpanda FM
13 June 2025, 5:12 pm

“Changamoto zilizopo ni kutokutekelezwa kwa sheria ya usalama mahala pa kazi”
Na Anna Mhina
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph amewataka wachimbaji wa madini kuzingatia sheria na miongozo ya uchimbaji ili kutosababisha madhara yanayoweza kuepukika.
Jamila ameyasema hayo kwenye kikao cha mafunzo ya wachimbaji yaliyofanyika katika ukumbi wa manispaa ya Mpanda na kusema kuwa miongoni mwa changamoto wanazokumbana nazo ni pamoja na kutokutekelezwa kwa sheria ya usalama na afya maeneo ya kazi.
Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya usalama na afya mahala pa kazi (OSHA) kanda ya nyanda za juu kusini Wilbert Ngowi ameeleza lengo la kuandaa mafunzo hayo kwa wachimbaji ni kuwapa uelewa wa jinsi ya kuboresha mazingira ya kazi.
Nao baadhi ya wachimbaji waliohudhuria mafunzo hayo wameeleza namna ambavyo mafunzo hayo yatakavyoleta mabadiliko katika shughuli zao za uchimbaji.
Zaidi ya wachimbaji wa madini 200 wameshiriki mafunzo hayo yaliyoandaliwa na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mpanda kwa kushirikiana na mamlaka ya usalama na afya mahala pa kazi (OSHA).