Mpanda FM
Mpanda FM
11 June 2025, 3:38 pm

Mkuu wa dawati la jinsia na watoto Katavi Judith Mbukwa. Picha na Anna Mhina
“Jinsi mtoto anavyotukanwa ndivyo atakavyokuwa”
Na Roda Elias
Kutokana na uwepo wa baadhi ya wazazi na walezi wa manispaa ya Mpanda mkoani Katavi kutumia lugha ya matusi kwa watoto imetajwa kuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili.
Wakizungumza na Mpanda Radio Fm wazazi hao wamesema kuwa katika maisha ya kila siku wazazi wamekuwa na desturi ya kuwatolea maneno yasiyofaa watoto ikiwemo kuwaita majina ya wanyama.
Kwa upande wake mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoani katavi Judith Mbukwa amesema kuwa kumtukana mtoto ni kumfanyia ukatili wa kijinsia hivyo wazazi waangalie adhabu za kuwaadhibu watoto.
Kwa upande wake mwanasaikolojia Rose Msabi amesema kuwa kuna viashiria mbalimbali vinavyoonyesha kuwa mtoto ameathirika kisaikolojia ikiwemo kutokuheshimu watu waliomzidi umri.