Mpanda FM
Mpanda FM
11 June 2025, 2:54 pm

Watangazaji wa Mpanda FM wakikabidhi moja ya taulo za kike. Picha na Samwel Mbugi
“Kuna haja ya kukiboresha chumba cha kujistiri kwa mtoto wa kike”
Na Edda Enock
Kuelekea madhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Mpanda Radio FM kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamegawa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike shule ya Rungwa Secondari pamoja na mpanda girls na baadhi ya wanafunzi kutokea shule mbalimbali mkoani Katavi na kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Meneja wa Mpanda Radio FM Denis Mkakala amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wa kituo hicho kusaidia jamii hasa watoto wa kike kwa kutoa elimu na kuwawezesha kupata vifaa vya kujisitiri wakati wa hedhi.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki zoezi hilo wamewashukuru Mpanda radio FM kwa kuwagawia taulo za kike huku wakisema kuwa elimu waliyoipata itawasaidia kuwa na ujasiri wa kuripoti matukio ya ukatili na kujitunza wakati wa hedhi.
Akizungumza kwa niaba ya mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Rungwa mwalimu Mackson Mapunda ameipongeza Mpanda radio FM kwa hatua hiyo waliyoifanya huku akisema kuwa ni hatua muhimu ya kuhamasisha usawa wa kijinsia na kuboresha mahudhurio ya wanafunzi wa kike shuleni wanapokuwa katika kipindi cha hedhi.
Utolewaji wa elimu ya ukatili wa kinjia shuleni hapo umefanywa na afisa ustawi wa jamii manispaa ya Mpanda na dawati la jinsia ambapo wamewataka wanafunzi hao kujiamini na kutoa taarifa pale wanapoona vitendo vya ukatili vikifanyika.