Mpanda FM
Mpanda FM
10 June 2025, 7:29 pm

Picha ya viongozi katikati ni mkuu wa mkoa wa Katavi mwanamvua Mrindoko. Picha na Samwel Mbugi
“Tuendelee kuchukua hatua zitakazotukinga na maradhi mbalimbali”
Na Samwel Mbugi
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka wananchi kuendelea kuchukua hatua za kujikinga na magonjwa ya mlipuko ikiwemo mafua makali.
Mrindoko ameyasema hayo kutokana na uwepo wa magonjwa ya milipuko ambapo amesema kila mwananchi anapaswa kujikinga na kuwalinda wengine wasipatwe na magonjwa hayo.
Pia ametumia nafasi hiyo kuwataka maafisa usafirishaji (bodaboda) kuwaelimisha abiria ambao wanatumia vyombo vyao kuhakikisha nao wanachukua tahadhari ili kutoambukizana.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni serikali ya Tanzania kupita wizara ya afya ilitangaza wananchi kuchukua tahadhari ya magonjwa ya mripuko ikiwemo ugonjwa wa Covid 19.