Mpanda FM

Ukarabati wa barabara Mpanda waathiri miundombinu ya maji

6 June 2025, 2:47 pm

Kaimu mkurugenzi MUWASA Rehema Nelson. Picha na Anna Mhina

“Wakarabati mabomba mana tunapata tabu”

Na Anna Mhina

Baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mpanda (MUWASA) kurekebisha miundombinu ya maji.

Wananchi hao wameeleza hayo kutokana na baadhi ya mabomba ya maji kupasuliwa kutokana na ukarabati wa barabara unaoendelea huku wengine wakiwa na mtazamo tofauti wakichukulia kama fursa kwao kupatikana kwa maji kwa urahisi.

Sauti za wananchi

Kwa upande wake kaimu mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mpanda CPA Rehema Nelson amesema  wanaendelea na ukarabati wa miundombinu hiyo licha ya ukarabati huo wa barabara umesababisha kuharibiwa kwa miundombinu ya maji.

Sauti ya kaimu mkurugenzi

Hata hivyo katika kuboresha huduma za maji mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Mpanda kwa mwaka wa fedha 2025/2026 wamepanga kufanya matengenezo km 15 maeneo yote ambayo yanachangamoto ya miundombinu ya maji.