Mpanda FM

Lipeni bili kwa wakati kuepuka usumbufu

5 June 2025, 6:31 pm

Kaimu mkurugenzi mtendaji MUWASA Rehema Nelson. Picha na Anna Mhina.

“Tutasitisha huduma za maji kwa wateja wasiolipa kwa wakati”

Na Leah Kamala

Kaimu Mkurugenzi mtendaji mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Rehema Nelson amewataka wananchi kuwa tayari kufikisha malalamiko yao ili yaweze kufanyiwa kazi.

Rehema amesema kuwa idara ya maji manispaa ya Mpanda iko tayari kushughulikia kero za wateja wa maji lakini pia wateja wapige simu kutoa malalamiko yao.

Sauti ya kaimu mkurugenzi

Aidha ameongeza kuwa wao kama mamlaka hawatosita kusitisha huduma ya maji kwa wateja wasiolipa kwa wakati hivyo amewataka wananchi kufuata utaratibu

Sauti ya kaimu mkurugenzi

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa manispaa ya mpanda mkoani Katavi wamesema kuwa wao kama watumiaji wa maji wana haki ya kufuata utaratibu Uliowekwa na mamlaka ili waweze kupata huduma iliyo bora.

Sauti ya wananchi