Mpanda FM
Mpanda FM
5 June 2025, 5:46 pm

Mratibu wa huduma ya macho dokta Japhet Chomba. Picha na Anna Mhina
“Tunaomba tupewe elimu ya lishe bora”
Na Anna Mhina
Baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wameiomba serikali iwape elimu ya kuwakinga watoto na ugonjwa wa macho.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wananchi hao wamesema kuwa hawana uelewa wa aina za vyakula wanavyopaswa kuwapa watoto hali inayopelekea watoto wengi kusumbuliwa na ugonjwa wa macho.
Kwa upande wake mratibu wa huduma ya macho katika hospitali ya Manispaa ya Mpanda Japhet Chomba amesema kuwa kutozingatia milo sahihi husababisha upungufu wa virutubisho kwenye macho.
Katika hatua nyingine dokta Chomba amesema ni jukumu la maafisa lishe kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii juu ya matumizi ya chakula bora chenye virutubisho vilivyojitosheleza.