Mpanda FM

EWURA yalegeza kamba uwekezaji vituo vya mafuta

4 June 2025, 9:47 am

Meneja wa EWURA mhandisi Walter Christopher . Picha na Leah Kamala

“Sisi kama EWURA tumelegeza masharti ili wawekezaji wawekeze vituo vya mafuta vijijini”

Na Leah Kamala

Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi  mhandisi Walter Christopher ametoa msisitizo umuhimu wa uvunaji wa maji ya mvua pamoja na usalama wa matumizi ya umeme.

 Ameyasema hayo katika semina iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo watendaji wa kata, wenyeviti wa mitaa pamoja na wenyeviti wa vijiji uliofanyika katika ukumbi wa mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda

Sauti ya mhandisi

 Aidha Mhandisi Christopher ameongeza kuwa wao kama mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji wamelegeza masharti ambayo yatawasaidia wananchi kuwekeza katika vituo vya mafuta katika maeneo ya vijijini

Sauti ya mhandisi

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) kanda ya Magharibi inayohudumia mikoa ya Tabora, Shinyanga, Katavi na kigoma ina jukumu la kusimamia  huduma za umeme, mafuta ya petroli, gesi asilia pamoja na maji katika mikoa hiyo.