Mpanda FM
Mpanda FM
4 June 2025, 9:31 am

“Hali ya barabara sio salama”
Na Samwel Mbugi
Baadhi ya wananchi wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio wamelalamikia ukarabati wa barabara za mitaa zilizorekebisha bila kumwagiwa maji wala kushindiliwa ambapo kumesababisha vumbi ambalo limekuwa kero.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wamemuomba mkandarasi aliyefanya kazi hiyo arudie kutengeneza ili ziwe bora kuliko zilivyo sasa.
Mwenyekiti wa mtaa huo Ivo Chambala amewaondoa wasiwasi wananchi kwa kusema kuwa ukarabati bado unaendelea kwa barabara zote ambazo zilikuwa hazipitiki baada ya mvua za masika kukata.
Ukarabati wa miundombinu ya barabarani unaendelea katika kata mbalimbali zinazopatikana manispaa ya Mpanda mara baada ya msimu wa mvua kutamatika.