Mpanda FM
Mpanda FM
2 June 2025, 12:26 pm

Picha ya matofali yaliyofyatuliwa kwenye makazi ya watu. Picha na Samwel Mbugi
“Hairuhusiwi kuchoma tofali katikati ya makazi ya watu”
Na Samwel Mbugi
Wananchi wanaojishughulisha na ufyatuaji tofali katika eneo la Mpanda hotel wametakiwa kuzingatia utaratibu na sheria za mazingira ili kuepukana na uharibifu unaoweza kujitokeza.
Mwenyekiti wa mtaa huo Ibrahim Ally Msanda amewataka wananchi wanaoruhusiwa kufyatua tofali ni wale ambao watapata kibali na kufuata sheria ya mazingira.
Aidha amesema hairuhusiwi kuchoma tofali katikati ya makazi hata kama umepata kibali cha kufyatua katika eneo lako kwani kuna maeneo rasmi yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli hiyo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi ambao wametembelewa na Mpanda radio FM katika shughuli zao za ufyatuaji tofali wamesema hawapo tayari kuzungumzia suala hilo.