Mpanda FM
Mpanda FM
26 May 2025, 1:20 pm

Mama lishe wilaya ya Tanganyika baada ya kupokea mitungi ya gesi. Picha na Eda Enock
“kumekuwa na ongezeko kubwa la ukataji miti mkoa wa Katavi kwasababu watu wengi hawajafikiwa na nishati safi”
Na Eda Enock
Wananchi mkoa wa Katavi wametakiwa kuepukana na matumizi ya nishati chafu ili kuepukana na hatari zinazoweza kuhatarisha afya na mazingira.
Ameyasema hayo Mbunge wa viti maalum mkoa wa Katavi Matha festo Maliki may 18/5/2025 ambapo ametangaza nia yake ya kuhamasisha kampeni ya Rais DKT. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya nishati safi kwa kugawa mitungi ya gesi kwa wajasiliamali wadogo maarufu kama Mama ntilie katika wilaya ya Mpanda na Tanganyika.
Kwa upande wao wajasiriamali wamemshukuru Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Katavi Matha Maliki kwa kuwapatia mitungi ya Gesi kwani ni hatua muhimu katika kuwapunguzia adha ya matumizi ya nishati hatarishi na kuboresha maisha ya wananchi.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alisema lengo la serikali ifikapo 2034 asilimia 80 ya watanzania watakua wanatumia nishati safi na salama ili kulinda ustawi wa afya za wananchi.