Mpanda FM
Mpanda FM
26 May 2025, 12:42 pm

“Msikitini hapa pana shule ya watoto wadogo ni vema kuchukua tahadhari na kila mtu kuwa mlinzi wa mwenzie”
Na Bertod Chove
Baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli za kilimo na ufyatuaji tofali katika moja ya bonde linalopatikana eneo la Kasimba Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wanahofia kuendelea na shughuli hizo mara baada ya kumuona nyoka aina ya chatu.
Wakizungumza na Mpanda radio fm wananchi hao wameiomba mamlaka kutatua changamoto hiyo ili waweze kuokoa mazao yao na kuendelea na shughuli za uzalishaji katika eneo hilo ili kujikimu kiuchumi na kupata chakula kwa ajili ya familia zao.
Kwa upande wake Bernad Nswima mwenyekiti wa mtaa wa Kasimba amesema katika jitihada za kutokomeza makazi ya nyoka amewataka wananchi ambao ni wamiliki wa viwanja katika eneo hilo kufanya usafi ili kutokomeza makazi ya nyoka hao.
Ikumbukwe miezi ya hivi Karibuni serikali kwa kushirikiana na wananchi katika eneo hilo walifanikiwa kuwauwa nyoka wawili aina ya chatu katika eneo hilo.