Mpanda FM
Mpanda FM
19 May 2025, 5:01 pm

‘lengo kuu la maadhimisho hayo ni kutambua mchango wa vyombo vya habari katika jamii ‘
Na Ben Gadau -Katavi
Kila mwaka, Mei 3 huadhimishwa kama Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Waandishi wa habari mkoani Katavi wameadhimisha siku hiyo mnamo Mei 13, kwa kuandaa hafla maalum ya utoaji tuzo kwa waandishi waliofanya kazi zenye kuleta matokeo chanya katika jamii.
Restuta Nyondo, akisoma risala kwa niaba ya waandishi, amesema lengo kuu la maadhimisho hayo ni kutambua mchango wa vyombo vya habari katika jamii huku akitoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana na wanahabari ili kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo nchini.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuph, amewataka wilaya ya Mpanda wadau wote kutoa ushirikiano kwa wanahabari ili kuhakikisha taarifa sahihi na zenye tija zinafika kwa wananchi na pamoja na kuchangia maendeleo.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo Buswelu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amehimiza waandishi wa habari kutumia kalamu zao kutangaza amani na kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.