Mpanda FM

Msimamo wa makatibu CHADEMA baada ya viongozi wa chama kujiudhuru

19 May 2025, 3:45 pm

picha na mtandao

Watahakikisha utawala bora na uwajibikaji ndani ya chama unakuwepo.

Na Edda Enock -Katavi

Makatibu wa chama cha demokrasia na maendeleo  CHADEMA mkoani Katavi wameweka wazi msimamo wao juu ya baadhi ya viongozi kujiudhuru ambapo wamesema kuwa watahakikisha utawala bora na uwajibikaji ndani ya chama unakuwepo.

Hayo yamejiri baada ya kujiudhuru Katibu wa CHADEMA mkoa wa katavi Erasto Julias Wegoro,ambapo  wamesema kuwa kujiudhuru kwake na  baadhi ya viongozi haijaleta athari yoyote katika chama hicho kwani chama kitaendea kubaki na kufanya uchaguzi wa viongozi wengine watakaokuwa na uzalendo wa CHADEMA.

Sauti ya makatibu chama cha CHADEMA

Aidha wamesisitiza kuwa wanachama wanatakiwa kuwa na msiamamo na kuhakikisha uchaguzi unakuwa na marekebisho ya kikatiba kwani katiba isipobadilishwa ni sawa na kuendelea na mfumo wa zamani ambao haujakidhi mahitaji ya chama hicho.

Sauti za makatibu wa CHADEMA

Makatibu hao wa CHADEMA ni makatibu wa wilaya tatu mkoani Katavi ambo ni katibu wa wilaya ya Mpanda Richadi Mponeja katibu wa wilaya ya Mlele Deus Kamoja katibu wa wilaya ya Tanganyika Stephano Masanja Ambapo wamesema kuwa wataendelea kusimamia msimamo wa NO REFORM,NO ELECTION.