Mpanda FM
Mpanda FM
3 May 2025, 12:56 pm

Picha ya Hassan Masanja mhandishi kitengo cha mafuta kanda ya magharibi. Picha na Anna Mhina.
“Hairuhusiwi kubeba mafuta kwenye madumu”
Na Rhoda Elias
Baadhi ya madereva wa vyombo vya moto wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi, hawana uelewa wa kutosha juu ya njia mbadala ya kifaa cha kubeba na kununulia mafuta.
Wakizungumza na Mpanda Radio FM Madereva hao wamedai kuwa, pindi vyombo vyao vya moto vinapoishiwa mafuta inawalazim kubeba kwenye maduka.
Hassan Masanja mhandishi kitengo cha mafuta kanda ya magharibi kutoka mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) amesema kuwa hairuhusiwi kubeba mafuta katika madumu badala yake ni kutumia vifaa maalumu vya kubebea mafuta.
Mnamo septemba 2024 mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA iltangaza katazo la kubeba na kuuza mafuta katika madumu.