Mpanda FM
Mpanda FM
1 May 2025, 1:52 pm

Picha ya wakuu wa shule za msingi Katavi. Picha na Samwel Mbugi.
“Jiwekeeni malengo ili mpandishe ufaulu”
Na Samwel Mbugi
Walimu wakuu wa shule za msingi mkoa wa Katavi wametakiwa kusimamia msingi wa utawala bora na uwajibikaji katika kazi ili kuleta tija ya ufaulu kwa wanafunzi.
Hayo yamesemwa na katibu tawala mkoa wa Katavi Albert Msovela ambae alikuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa TAPSHA uliofanyika shule ya Sekondari Nsimbo ukijumuisha walimu wakuu wa shule za msingi.
Kwa upande wake afisa elimu mkoa wa Katavi Dafrosa Ndalichako amesema kuwa walimu wanatakiwa kujiwekea malengo na kujitathimini ili kupandisha matokea ya ufaulu kwa wanafunzi.
Mwenyekiti wa umoja wa walimu wakuu TAPSHA mkoa wa Katavi Keneth Sichalwe amesema kuwa maagizo yote yaliyoagizwa na katibu tawala wataenda kuyatekeleza na kuinua ufaulu kwa wanafunzi kama ilivyoagizwa.