Mpanda FM
Mpanda FM
1 May 2025, 1:30 pm

Picha ya baraza la madiwani Tanganyika. Picha na Beny Gadau
“Tumemuondoa daktari wa Mchangani amekuwa na uwajibikaji hafifu”
Na Beny Gadu
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Tanganyika wamefanya kikao cha robo ya kwanza kwa mwaka 2025 chenye lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo katika wilaya hiyo.
Wakizungumza baadhi ya madiwani katika kikao hicho wamemuomba mwenyekiti wa halmashauri hiyo pamoja na Mkurugenzi kutatua baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikikwamisha baadhi ya miradi ya maendeleo kuendelea.
Akijibia baadhi ya changamoto mkurugenzi wa halmashauri hiyo Shabani Juma amesema kuwa katika kuhakikisha miradi ya kimaendeleo inakamilika kwa wakati wamemchukulia hatua za kumuondoa kazini daktari wa zahanati ya Mchangani kata ya ikola ambaye amekuwa na uwajibikaji hafifu kwa wananchi na usimamizi wa miradi ya serikali.