Mpanda FM
Mpanda FM
30 April 2025, 10:33 am

Picha ya mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Asina Omari. Picha na John Benjamin
“Tekelezeni zoezi hilo kwa umakini”
Na John Benjamin
Maafisa uchaguzi ngazi ya kata wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuhakikisha wanasimamia kanuni na sheria katika zoezi la uandikishaji wa daftari la mpiga kura.
Hayo yamebainishwa na mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama Kuu, Asina Omari katika ufunguzi wa mafunzo kwa maafisa uchaguzi ngazi ya kata manispaa ya Mpanda ambapo ameleeza kuwa kila mmoja anapaswa kutekeleza zoezi hilo kwa umakini na kuhakikisha hakuna changamoto yoyote inajitokeza.
Afisa uchaguzi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Deudatus Kangu amewataka maafisa uchaguzi kusimamia majukumu yao ya uandikishaji wa daftari la mpiga kura kwa weredi bila ubaguzi wa vyama vya kisiasa, udini wala ukabila
Kwa upande wao baadhi ya waandikishaji ngazi ya Kata waliokuwa wakipatiwa mafunzo hayo wameahidi kwenda kutenda haki kwa kusimamia na kutekeleza yale walioyoagizwa na kufundishwa kuhakikisha zoezi hilo linakamilika kwa ufasaha
Mei mosi kunatarajiwa kuanza zoezi la uandikishaji wa daftari kwa ajili ya mpiga kura kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi wa 10 mwaka huu.