Mpanda FM
Mpanda FM
29 April 2025, 1:12 pm

Picha ya Afisa NIDA Katavi Mauna Karumbeta. Picha na Samwel Mbugi
“Namba zinaenda kufutiwa usajili ni zile zilizotumiwa ujumbe”
Na Samwel Mbugi
Baadhi ya wananchi mkoani Katavi wametoa maoni mseto kuhusiana na zoezi la kufutiwa usajili wa namba za nida ambazo vitambulisho vilishatoka lakini havijachukuliwa.
Wakizungumza na Mpanda radio FM wamesema kuwa serikali iongeze muda ili wananchi ambao hawana taarifa ziweze kuwafikia na kuchukua vitambulisho vyao.
Kwa upande wake afisa wa NIDA mkoa wa Katavi Mauna Karumbeta amesema kuwa namba ambazo zinaenda kufutiwa usajili ni zile zilizotumiwa ujumbe kutokana na wahusika kushindwa kuchukua vitambulisho .
Karumbeta ameongeza kuwa vitambulisho hivyo ni vile ambao vilitoka kuanzia mwaka 2019 hadi 2023 na kutokuchukuliwa na wahusika vitahusika katika ufutwaji wa usajili .
Ikumbukwe kuwa ukiwa na namba au kitambulisho cha nida kinakusaidia kupata huduma nyingi za kijamii, kiuchumi na kiusalama.