Mpanda FM
Mpanda FM
22 April 2025, 6:56 pm

Picha ya Makamu Askofu wa kanisa la Roman Cathoric Katavi. Picha na Anna Mhina
“Tumepokea kifo cha baba mtakatifu kwa mshtuko na ameacha pengo”
Na Anna Mhina
Waumini wa kanisa la Roman Cathoric mkoani Katavi wametakiwa kushikamana katika kipindi hiki kigumu na kumuombea baba mtakatifu Papa Francis ambaye ametangulia mbele za haki.
Akizungumza na Mpanda radio FM Makamu Askofu wa kanisa la Roman Cathoric mkoa George Kisampa amesema habari za kifo cha Papa Francis wamekipokea kwa mshtuko na kueleza pengo aliloliacha.
Kwa upande wao baadhi ya waumini wa kanisa hilo wameeleza namna walivyoguswa na msiba huo na kuahidi kuyaishi yale yote yaliyokuwa yakihubiriwa na Papa Francis ikiwemo kudumisha amani.
Papa Francis alichaguliwa kuwa Papa March 13, 2013 akiwa na umri wa miaka 76 na kufariki April 21, 2025 akiwa na umri wa miaka 88.