Mpanda FM
Mpanda FM
19 April 2025, 7:16 pm

Picha ya mchungaji Paul Mahenenga. Picha na Anna Mhina
“Acheni kuhangaikia mavazi na vyakula”
Na Anna Mhina
Waumini wa imani ya makanisa ya kipentekoste mkoani Katavi wametakiwa kuacha kuhangaikia mambo ya kimwili katika kuadhimisha siku ya Ijumaa kuu ambayo ni kumbukizi ya mateso ya Bwana Yesu Kristo.
Akizungumza kwa niaba ya Askofu wa mkoa mchungaji Paul Mahenenga amesema wakristo wanapaswa kutofautisha siku ya leo na sherehe ya mwaka mpya kwa kujali mambo ya kiroho na kuacha kuhangaikia mavazi na vyakula.
Kwa upande wao baadhi ya waumini wamesema kuwa watendeleza matendo mema na toba kama ilivyokua katika kipindi chote cha Kwaresma.
Wakristo duniani kote wanatarajia kusheherekea sikuku ya Pasaka April 20 mwaka huu ambayo ni kumbukizi ya kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo.