Mpanda FM

Laki moja yazua utata msibani Katavi

5 April 2025, 9:38 pm

Baadhi ya wananchi waliojetokeza katika mazishi

“Wameshtushwa na kadhia hiyo ya uongozi wa dini hiyo kutaka kulipia pesa ili waweze kumstiri ndugu yao”

Na Ben Gadau -Katavi

Hali ya sintofahamu imeibuka katika kijiji cha Mtakuja baada ya baadhi ya wananchi kudaiwa kulipa kiasi cha shilingi laki moja kwa uongozi wa dini ya kiislamu wa eneo hilo ili waweze kufanya mazishi.

Wakizungumza katika eneo hilo baadhi ya wananchi hao wamesema wameshtushwa na kadhia hiyo ya uongozi wa dini hiyo kutaka kulipia pesa ili waweze kumstiri ndugu yao huku wakiiomba serikali kulifanyia kazi jambo hilo.

Saiti za baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mazishi

Kwa upande wake Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mashaka Kakulukulu akizungumza kwa njia ya simu amekiri kuwepo kwa waraka unaobainisha kulipwa kwa kiasi hicho kwa ajili ya mazishi huku akiwataka wananchi kuwa watulivu wakati akiendelea kufanya uchunguzi juu ya suala hilo kubaini namna lilivyotekelezwa katika eneo hilo.

Sauti ya Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Katavi akizungumza

Licha ya sintofahamu hiyo mwili wa marehemu huyo umepumzishwa katika nyumba yake ya milele.