

5 April 2025, 9:11 pm
“Mkoa wa Katavi una changamoto ya udumavu kwa asilimia 32%.”
Na Samwel Mbugi- Katavi
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Hozza Mrindoko amewasisitiza wananchi kuzingatia lishe bora kwa kuzingatia makundi sita (6) ya chakula ili kuondokana na udumavu.
Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya lishe bora iliyozinduliwa April 05,2025 katika ukumbu wa manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi, ambapo amesema mkoa wa katavi una changamoto ya udumavu kwa asilimia 32%.
Awali Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Albert Msovela akiwasilisha taarifa kwa mgeni rasmi amesema kuwa watahakikisha elimu ya lishe bora inatolewa kwa wananchi kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo kutumia vyombo vya habari.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Katavi Idd Kimanta amesema kuwa wataungana na uongozi wa serikali katika kuhakikisha kampeni ya lishe bora inafanikiwa.
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni viongozi mbalimbali wa mkoa wa katavi walienda mkoa wa Njombe kwenda kujifunza namna gani wao wameweza kukabiliana na changamoto ya udumavu. na kauli mbiu ya kampeni hiyo ni Lishe bora, afya yako,zingatia unachokula.