

31 March 2025, 1:47 pm
“Amani ndio msingi wa maendeleo tuilinde katika mambo yote kama hakuna amani ni ngumu kufanyika chochote, tuendelee kuiombea nchi yetu amani”
Na Samwel Mbugi-Katavi
Wananchi mkoani katavi watakiwa kuitunza amani iliyopo kwani ndio jambo lakwanza kabisa kabla ya mambo yote na ikipotea ni kazi kubwa sana kuirudisha.
Hayo yamesemwa na Sheikh mkuu wa Mkoa wa Katavi Mashaka Nassor Kakulukulu wakati akizungumza na waamini wa dini ya kiisilamu siku ya kuazimisha sikukuu ya eid al Fitr iliyofanyika katika viwanja vya kashato manispaa ya Mpanda.
Pia kakulukulu amesema kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wananchi wanapaswa kuwa makini na baadhi wa wanasiasa ambao watakuwa na kauli mbalimbali ambazo zinaweza kuchochea uvunjifu wa amani.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka wananchi wa mkoa wa Katavi kusherekea sikukuu ya eid kwa amani na usalama kwani wamejipanga kuhakikisha utulivu unakuwepo.
Hata hivyo Mwanamvua ametoa shukrani kwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani.