

26 March 2025, 3:43 pm
“Taifa linahitaji nguvu kazi ya vijana”
Na John Benjamin
Vijana mkoani Katavi wameombwa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi mbalimbali katika uongozi wa kisiasa
Hayo yamezungwa na mwenyekiti wa ngome ya vijana wa chama cha ACT Wazalendo mkoa wa Katavi ambapo amesema kuwa taifa linahitaji nguvu kazi ya vijana na kuwaomba vijana kujitokeza kuwania nafasi mbali mbali bila kujali vyama vyao
Aidha amesema kuwa chama cha ACT Wazalendo kinaendelea kujipanga kuhakikisha kinaendelea kutoa nafasi za vijana kujiunga na kuwania nafasi mbali mbali za uongozi kupitia chama hicho
Chama cha ACT Wazalendo tarehe Apr 1 mwaka wa huu kinatarajia kufanya uzinduzi wa kampeni yake ya Oparesheni linda Demokrasia kuelekea uchaguzi mkuu.