

25 March 2025, 9:39 am
Wajumbe wa CCM wakipokea mfuko mmoja wa saruji kwa niaba ya mifuko 40. Picha na Anna Mhina
“Lengo la kutoa mifuko hiyo ni kukifanya chama kionekane cha tofauti”
Na Anna Mhina
Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Haidary Sumry ametoa mifuko 40 ya saruji kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi za chama cha mapinduzi ( CCM) ngazi ya kata.
Akikabidhi mifuko hiyo kwa wenyeviti wa kata wa chama hicho ikiwemo kata ya Kawajense na katika ofisi ya tawi la Kilimani lililopo kata ya Nsemulwa Sumry amesema lengo la kutoa mifuko hiyo ni kukifanya chama kionekana cha tofauti kwa kuboresha mazingira katika ofisi za kata.
Kwa upande wao baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi(CCM) ngazi ya kata wamemshukuru mstahiki meya kwa kuwapatia mifuko ya saruji itakayosaidia katika ujenzi unaoendelea na kuwaomba wadau wengine kujitokeza ili kukamilisha ujenzo huo.
Ujenzi wa ofisi za chama cha mapinduzi katika kata ni utekelezaji wa agizo la mwenyekiti wa chama mkoa Idd Kimanta pindi alipoingia madarakani.