

14 March 2025, 6:08 pm
Picha ya Leonard Minja afisa TAKUKURU Mpanda. Picha na Anna Mhina
“Msichague viongozi watoa rushwa”
Na Anna Mhina
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Katavi imewataka wananchi kuchagua viongozi kutokana na ushawishi wa sera na ilani za vyama vyao ili kuleta maendeleo.
Akizungumza na Mpanda radio FM afisa wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mpanda Leonard Minja amewataka wananchi wasichague viongozi watoa rushwa kwani ni kikwazo katika maendeleo.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Mpanda wameeleza madhara ya rushwa katika kuchagua viongozi ikiwemo kuwepo kwa huduma duni za kijamii.
Haya yanajiri wakati Tanzania ikiwa katika maandalizi ya kufanya uchaguzi mkuu wa madiwani,wabunge na Raisi unaotarajiwa kufanyika mwezi October mwaka huu.