

11 March 2025, 4:28 pm
Picha ya madereva bodaboda. Picha na Edda Enock
“Waliochaguliwa watimize ahadi walizotuahidi”
Na Edda Enock
Maafisa usafirishaji bajaji manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamefanya uchaguzi wa viongozi kwa ngazi mbalimbali.
Akitangaza matokea ya uchaguzi huo mwenyekiti wa uchaguzi huo Mrisho Seleman Ally amesema kuwa nafasi ya ukatibu Kulikua na wagombea wawili ambao ni Hamidu Selemani ambae amepata kura 31 na Magullat John ambae amepata kura 304, na kwa upande wa uenyekiti wagombea walikua wawili ambao ni Aden Sandanda ambae ameibuka na kura 255 na Boniface Mayanga ameibuka na kura178 na kumtangaza Aden Sandanda kuwa mshindi wa uenyekiti wa usafirishaji manispaa ya Mpanda.
Kwa upande wake mwenyekiti mpya wa usafirishaji bajaji manispaa ya Mpanda Aden Sandanda amewashukuru waendesha bajaji kwa kumpatia kura na kauhidi kufanya kazi kwa kushirikiana na waendesha bajaji wote kwa maslahi mapana na kutekeleza yale yote aliyowaahidi.
Boniface Mayanga Ambae ni moja ya wagombea waliokuwa wakigombea nafasi ya uenyekiti wa maafisa usafirishaji amekubaliana na matokea yaliyotangazwa na kusema kuwa uchaguzi ulikuwa wa huru na haki na kueleza kuwa wapo tayari kushirikiana na Washindi hao.
Uchaguzi huo umefanyika tarehe 7/3/2025 na matokeo yametangazwa soko kubwa stendi ya bajaji ambapo jumla ya watu waliopiga kura ni 335.