

13 February 2025, 12:02 pm
“huwa hawazui miili ya marehemu bali kuna taratibu za kufuata kutokana na pesa ambazo serikali zimewekeza kwenye sekta ya afya.“
Na Lilian Vicent -Katavi
Baadhi ya wenyeviti wa mitaa mkoani Katavi wameeleza taratibu ambazo wanachukua iwapo ikitokea mwananchi ambaye ameshindwa kuchukua mwili wa marehemu kutokana na kushindwa kumudu gharama zilizotumika kwa ajili ya matibabu.
Wakizungumza na Mpanda Redio FM wamesema kuwa wao kama viongozi wanaoaminiwa na wananchi wamekuwa wakihusika katika kuthibitisha utambulisho wa watu hao.
Akizungumza na Mpanda Radio FM Mganga mfawidhi wa hospitali ya Rufaa mkoa wa Katavi Banuba Deogratis amesema kuwa huwa hawazui miili ya marehemu bali kunataratibu za kufwata kutokana na pesa ambazo serikali zimewekeza kwenye sekta ya afya.
Deogratis ameongeza kuwa zaidi ya million ishirini mpaka sasa hazijalipwa na watu waliopewa huduma lakini asilimia kubwa wananchi wengi wakishapewa kibali cha kuzika huwa hawalipi fedha hizo.