

13 February 2025, 11:22 am
amefariki baada ya kupigwa na Sungusungu kwa tuhuma za kushukiwa anajishughulisha na vitendo vya wizi.
Na Betold Chove -Katavi
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amekemea vitendo vya Wananchi kujichukulia sheria mkononi, hali inayopelekea uvunjifu wa amani na kuhatarisha maisha ya raia wengine.
Buswelu ameyasema hayo katika Kijiji cha Vikonge alipohudhuria mazishi ya Mwananchi Mmoja, aliyefahamika kwa jina la Justine (28), ambaye alifariki baada ya kupigwa na Sungusungu kwa tuhuma za kushukiwa anajishughulisha na vitendo vya wizi.
Kwa upande wake mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Tanganyika, OCD P. Mashimbi amesisitiza kuwa sheria za nchi haziruhusu Wananchi kujichukulia sheria mkononi.